TET, TSLTDO zasaini ushirkiano lugha ya alama

DAR ES SALAAM; TAASISI ya Elimu Tanzania (TET), imesaini makubaliano ya ushirikiano (MOU)  ya kutafsiri lugha ya alama na Shirika la Maendeleo ya Utafsiri wa Lugha ya Alama Tanzania  (TSLTDO) maarufu BILAT.

Mkurugenzi wa TET,  Dk Aneth Komba, amesema jukumu la taasisi yake katika makubaliano hayo ni kuipatia TSLTDO nakala laini ya vitabu vyote vya kiada vinakavyopaswa kutafsiriwa katika lugha ya alama.

Pia itawakutanisha TSLTDO na wakuza mitaala kwa ufafanuzi wa jambo lolote, iwapo itahitajika kufanyika hivyo.

“TET itatoa usaidizi wa kitaalamu katika kutathmini usahihi wa ufasiri wa vitabu uliofanywa na TSLTDO kadri itakavyohitajika,” amesema.

Pia amesema TET itatoa fedha zitakazowezesha kukamilisha kazi ya kutafsiri vitabu vya kiada kwa mujibu wa taratibu na kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha.

Kwa upande wa Rais wa BILAT, Mchungaji Joseph Msimbete, amesema Jamii ya Viziwi ndio kundi kubwa zaidi, ambalo halijafikiwa katika masuala mengi kutokana na vikwazo vya mawasiliano.

” Hali hii inasababishwa na elimu duni, kukosa ajira za kueleweka, mwamko  hasi kwa jamii kuhusu viziwi na kuishia maisha ya udhalili,” amesema Msimbete na kuongeza:

” Kwa upande wa elimu, watoto wengi viziwi nchini wanaanza shule bila kujua lugha yoyote rasmi…lugha ya kwanza kukutana nayo ni Kiswahili, lugha ambayo wengi wao ni ngeni hawajawahi kuisikia wala kuifahamu,” amesema.

Amesema viziwi wanapomaliza elimu ya msingi wanakwama kusonga mbele na kupambania ndoto zao kwa kuwa dunia inahitaji mawasiliano na elimu ya kutosha, ili kumwezesha mtu kimaisha.

“Hivyo ujio wa vitabu vya kidijitali vilivyo katika lugha ya alama ni moja ya suluhu ya kukabiliana na changamoto hizo,” amesema Msimbete

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
LiliaHood
LiliaHood
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by LiliaHood
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x