TET yazindua maabara, yakabidhi vifaa vya Tehama

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imezindua Maabara katika shule ya Sekondari Kimbiji Kigamboni jijini Dar es salaam sambamba na kukabidhi vifaa vya Tehama kutoka nchini Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean e-learning Improvement Cooperation 2022).
KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na nchi ya Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia ya mtandao kwa Walimu 20 shule ya sekondari kimbiji.
Akizungumza wakati, Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt.Aneth Komba amemshukuru Rais wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya Elimu nchini ambapo ameeleza kuwa walimu katika shule hiyo wataweza kutekeleza kwa urahisi kazi ya ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya kieletroniki.
Amewataka walimu wa shule hiyo kuhakikisha wanatumia fursa ya uwepo wa vifaa vya TEHAMA na mafunzo waliyoyapa kuendelea kuboresha mbinu za ujifunzaji na ufundishaji ili kuinua ubora wa elimu.
“Uongozi wa shule uweke ratiba nzuri ya kuwawezesha wanafunzi kwa usimamizi wa karibu wa walimu wapate fursa ya kutumia vifaa hivi kama sehemu ya utekelezaji wa Mtaala kwa vitendo hasa katika somo la Sayansi na Teknolojia”. Amesema
Aidha ameomba uongozi wa shule kuhakikisha vifaa hivi vinatumika vizuri, vinatunzwa pamoja na kuhakikisha vinalindwa visiibwe wala kutokea upotevu wa aina yoyote.
Hata hivyo amesema TET inaamini kuwa kushiriki kwa Shule ya Sekondari Kimbiji katika mradi wa KLIC kutaleta matokeo chanya katika kuboresha na kuendeleza matumizi sahihi ya elimu mtandao nchini hivyo kuifanya shule hii kuwa ni shule ya mfano katika matumizi ya TEHAMA katika elimu ndani ya Halmashauri ya Ubungo na hatimaye taifa kwa ujumla.
“TET itaendelea kutoa ushirikiano kwa kuitembelea shule ya Sekondari Kimbiji na kutoa mafunzo ya kazini kuhusu utunzaji wa vifaa na namna ya kutumia TEHAMA kuboresha zoezi zima la ujifunzaji na ufundishaji kwa kadri nafasi itakapokuwa inapatikana”. Amesema
Tukio hilo liliambatana na kuwapatia zawadi walimu walioshiriki mafunzo hayo vishikwambi 20.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Kimbiji Bw.Joseph Kiseke ameshukuru kwa uzinduliwa wa maabara hiyo ya TEHAMA na kukabidhiwa vifaa vyote huku akieleza kuwa atahakikisha vinatumika ipasavyo katika kuboresha elimu.
Kwa upande wao baadhi ya walimu waliopatiwa vifaa hivyo vya tehama wamesema vitakuwa msaada kwao kwani vitawarahisishia katika kufundisha wanafunzi kwa urahisi.
Vifaa vilivyokabihiwa ni pamoja na ‘UPS 26, computure Monitor 25, system Unit 25, Wirless keyboard 35, projector moja, scanner moja, printer moja, wireless mouse 35, headphone 25, electric blackboard moja, webcamera 26, digital podium moja, wired keyboard 25,wired mouse 25, speaker 26, adapter 49 na usb flash disk 50’

Habari Zifananazo

Back to top button