Tetemeko lingine laua Uturuki
Watu watatu wamefariki na wengine kujeruhiwa kufuatia tetemeko jipya la ardhi lililotokea Uturuki na Syria usiku wa leo.
Tetemeko hilo limetokea Mkoa wa Hatay nchini Uturuki. Imeelezwa kuwa watu wasiopungua watatu wameuawa na zaidi ya 200 walijeruhiwa na walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Waziri wa mambo ya ndani nchini Uturuki Süleyman Soylu amesema hayo baada ya matetemeko mawili kutokea, tetemeko la kwanza liliripotiwa kuwa na ukubwa wa 6.4 kwenye vipimo vya ritcha na la pili lililotokea dakika tatu baadaye, nalo lilikuwa na ukubwa wa 5.8 kwenye vipimo vya ritcha.
Janga hilo limetokea kwa mara ya pili ikumbukwe Februari 6, 2023 lilitokea tetemeko katika nchi hizo na kuuwa watu zaidi ya 47,000 na kuwaacha zaidi ya milioni 2 wakiwa hawana pakuishi.