Tetesi za soka Ulaya

MSHAURI wa soka Paris St-Germain (PSG), Luis Campos amezungumza na wakala wa Jose Mourinho kuhusu uwezekano wa meneja huyo wa Roma kuchukua mikoba msimu huu wa joto. (RMC Sport – kwa Kifaransa).

Mshambulaiji, Lionel Messi, ambaye mkataba wake na PSG unamalizika majira ya joto, bado hajafikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia. (Mundo Deportivo).

Messi 35, anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake mara tu msimu utakapokamilika Juni 3, 2023 (Mundo Deportivo )

Chelsea wanapanga kumtoa Christian Pulisic, 24, mwishoni mwa msimu huu na wanaweza kumtumia kama uzani kuitaka Napoli kumuuza mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24. (Mail).

Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza, Jude Bellingham, 19, atakataa ofa ya kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja hadi 2026 na mshahara ulioboreshwa zaidi wa euro 14m baada ya taarifa ya kuhamia Real Madrid (Bild in Germany).

Barcelona wameweka bei inayotakiwa ya euro 80m (£70m) kwa winga wa Brazil Raphinha, 26, ambaye anasakwa na Newcastle United na Chelsea.(Sport-in Spanish).

Bayer Leverkusen wamefufua nia yao ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 30, baada ya kushindwa kumsajili msimu uliopita (Mirror).

West Ham wapo tayari kumuachia kiungo Mwingereza Declan Rice mwenye umri wa miaka 24 msimu huu ikiwa watapokea ofa nzuri. (Mail)

Kiungo wa kati wa Marseille na Ufaransa Matteo Guendouzi, 24, ni chaguo kwa West Ham kama mbadala wa Rice endapo ataondoka. ( Athletic)

Eintracht Frankfurt haitamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 24, kwa chini ya euro 90m (£79m). (Football 90)

Winga wa Crystal Palace, Michael Olise, 21, anavutiwa na Paris St-Germain, wako tayari kutuma ofa ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 msimu wa joto. (Mail)

Aston Villa, Leeds United na West Ham wamehusishwa na mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele, 26. (Mail Birmingham).

Kipa wa Hispania, David de Gea, 32, hajahakikishiwa kuendelea kuwa chaguo la kwanza la Manchester United msimu ujao, ingawa anakaribia kuafiki mkataba mpya. (Telegraph)

Mkurugenzi wa michezo wa Newcastle United, Dan Ashworth na skauti Mick Tait wanamfuatilia kiungo wa kati wa Blackburn Rovers Muingereza Adam Wharton, 18. (Mail)

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button