TETESI ZA USAJILI ULAYA

Habari za wakati huu mdau wa michezo, popote pale unapotufuatilia kupitia mitandao yetu, ikiwa ni Januari 2, 2023 karibu sana tukupitishe katika tetesi za usajili barani Ulaya huku dirisha la usajili likiwa limefungulia.

Miongoni mwa yale utakayoyasoma mchana huu ni kuhusiana na sajili za Arsenal, Manchester United.

Chelsea wanajipanga kufanya jaribio la mwisho kwa Shakhtar Donetsk juu ya kumsajili winga wa Ukraine Mykhailo Mudryk, licha ya The Gunners kuwa tayari wameafikiana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (The Sun ).

Advertisement

Chelsea wanasita kutoa Euro 120m (£105.8m) iliyopo katika mkataba (release Clause) wa kiungo wa kati wa Benfica, Enzo Fernandez 21, ambao wanataka ada hiyo ilipwe kikamilifu ili kukubali uhamisho wake. (Telegraph ).

Kiungo wa kati wa Uholanzi Memphis Depay amekuwa akihusishwa kurejea Manchester United lakini mkufunzi wa Barcelona Xavi anataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 abaki Nou Camp. (Metro).

Manchester United bado wanaweza kumuuza beki wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka mwezi Januari, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuonyesha kiwango kizuri hivi karibuni. ( Athletic).

Brentford wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Kevin Schade kwa £22m kutoka Freiburg baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kufaulu vipimo vya afya. (Times – subscription required)

Mshambulizi wa Brentford mwenye umri wa miaka 21 kutoka Scotland Aaron Pressley amekubali mkataba wa kujiunga na Accrington Stanley kwa mkopo. (Football Insider)

Chelsea, Newcastle United na Bayern Munich wanavutiwa na kipa wa Leeds United Illan Meslier, lakini klabu hiyo ya Elland Road haitaki kumuuza Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22. (RMC Sport – kwa Kifaransa)

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers bado anatumai kuwa klabu hiyo inaweza kukubaliana mkataba mpya na kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, ambaye mkataba wake utakuwa nje ya msimu wa joto. (Goal)

Arsenal wako tayari kumuuza beki wa kulia wa Ureno Cedric Soares, lakini uhamisho wa kwenda Fulham unazuiliwa na matakwa ya mshahara ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31. (Evening Standard).

1 comments

Comments are closed.