Tetesi za usajili Ulaya

IMERIPOTIWA Liverpool ipo tayari kutoa Pauni £70m kwa ajili ya kunasa saini ya kiungo wa Brighton, Alexis Mac Allister. Chanzo (Mirror).

Mauricio Pochettino, ambaye amekubali kufundisha Chelsea anataka kiungo Mason Mount aendelee kubaki klabuni hapo ingiwa kiungo huyo 24, amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake. Chanzo (The Mail).

Chelsea ipo tayari kuweka mezani pauni £70m kwa ajili ya kumbeba kiungo wa Brighton Moise Caicedo msimu huu.

Chanzo (Fichajes – in Spanish).

Manchester City na Kyle Walker, 32, wapo tayari kuachana na ofa kutoka vilabu vingine na kukaa meza moja kwa ajili ya kubali Etihad. Chanzo (Sun).

United na beki wao Lisandro Martinez wapo kwenye mstari mmoja wa makubaliano ya nyongeza ya mshahara. Chanzo (The Sun).

Everton huenda ikawa ipo tayari kupokea paundi £50m kwa ajili ya kumuachia Amadou Onana endapo tu wakishuka daraja. Chanzo (Football Insider).

Barcelona imevutwa na huduma ya kiungo wa Wolves Ruben Neves na sasa wanajipanga kutaka huduma yake.

Chanzo ( TalkSPORT).

Aston Villa inataka saini ya kiungo wa Madrid, Marco Asensio, 27, na kiungo wa Barcelona Ferran Torres. Chanzo (Sport-in Spain).

Habari Zifananazo

Back to top button