Tetesi za usajili Ulaya

PARIS Saint Germain wamempa kipaumbele mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane, 29, msimu huu baada ya kuondoka mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35. (Le Parisien – Uifaransa).

Beki wa Uingereza Kyle Walker, 33, yuko kwenye mazungumzo juu ya kuongezewa mkataba katika klabu ya Manchester City licha ya kutakiwa na Bayern Munich. (Mail).

Kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 28, amepokea ofa ya kujiunga na Saudi Pro League. (Athletic).

Advertisement

Mabingwa wa Saudi Pro League Al-Ittihad wanatayarisha ofa ya pauni milioni 51 kwa mshambuliaji wa Tottenham mwenye umri wa miaka 30 kutoka Korea Kusini Son Heung-min.(ESPN).

Kiungo wa kati wa West Ham na Uingereza Declan Rice, 24, yuko tayari kukubaliana masuala binafsi na kuwa mchezaji wa Arsenal mwezi huu. (Mail)

Tottenham wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa kati wa Leicester na England James Maddison, 26, ambaye anapendelea kuhamia London badala ya Newcastle.(Northern Echo).

Mshambulizi wa Uingereza Marcus Rashford, 25, yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa muda mrefu katika klabu ya Manchester United. (Mail)

Mshambuliaji wa Ujerumani Kai Havertz hana nia ya kusaini mkataba mpya Chelsea. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 analengwa na Arsenal. (ESPN).