Tetesi za usajili Ulaya

Manchester City wamewasilisha dau la Euro 90m (£77m) kwa Josko Gvardiol wa RB Leipzig, 21, huku beki huyo wa Croatia akitajwa kama “mchezaji ndoto” wa Pep Guardiola. (Sky Sport Ujerumani)

Mshambulizi wa Villarreal na Senegal, Nicolas Jackson, 22, anatazamiwa kukamilisha uhamisho wa Euro 35m (£30m) kwenda Chelsea baada ya kukamilisha vipimo vya afya jana. (Athletic – subscription required)

Mikel Arteta anasema anafuraha Arsenal na amepuuza ripoti zinazomhusisha na Paris St-Germain. (Marca).
Klabu ya Al-Hilal inataka kumsajili winga wa Jamaica Demarai Gray, 26, kutoka Everton, huku mazungumzo yakipangwa kufanyika wiki ijayo. (Mail)

Beki wa kati wa Colombia Yerry Mina, 28, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Everton mwishoni mwa msimu huu, anatarajiwa kusajiliwa na Fulham. (Sun)

Al-Nassr wanatumai kukamilisha dili la winga wa Chelsea kutoka Morocco Hakim Ziyech, 30, mapema wiki hii, na kumfanya kuwa mchezaji wa nne kuondoka Stamford Bridge kwenda Saudi Arabia msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Manchester United, Erik ten Hag ataruhusu wachezaji 11 kuondoka Old Trafford msimu huu wa joto huku akiomba zaidi ya pauni milioni 100 kusaidia kubadilisha kikosi chake. (sun)

Man United inamtazama kiungo wa kati wa Ajax na Ghana Mohammed Kudus, 22, na mchezaji wa kimataifa wa Utrecht wa Marekani Taylor Booth, 22, baada ya kushindwana na Chelsea kuhusu mpango wa kumnunua Mason Mount. (ESPN)

Mkufunzi wa Bayern Munich Thomas Tuchel anatamani kuungana tena na kiungo wa kati wa Uingereza Mount, 24, ambaye alikuwa akimfundisha Stamford Bridge. (The Guardian)

Liverpool wanajipanga kushindana na Tottenham kumnunua mlinzi wa Uholanzi Micky van de Ven, 22, ambaye yuko tayari kuondoka Wolfsburg msimu huu wa joto. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Uturuki Arda Guler, 18, anavutiwa na Arsenal, Liverpool, Real Madrid na Benfica (Record – in Portuguese)

Gerardo ‘Tata’ Martino, ambaye amewahi kumfundisha Lionel Messi huko Barcelona na Argentina, anaweza kuwa kocha wake kwa mara ya tatu baada ya kufanya mazungumzo ya kuchukua mikoba ya mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 36 katika klabu mpya ya Inter Miami. (Athletic – subscription required)

Fulham wamefanya mpango wa kumsajili fowadi wa Marekani Brenden Aaronson, 22, kwa mkopo kutoka Leeds United. (Mail)

Habari Zifananazo

Back to top button