Tetesi za usajili Ulaya
BAYERN Munchen wanapanga kuwasilisha ofa ya pili kwa Tottenham kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa England, Harry Kane. (Sky Sport)
Manchester City wanajiandaa kupeleka ofa kwa ajili ya kumnasa beki Mcroation, Josko Gvardiol, 21, baada ya kuanza mazungumzo rasmi na RB Leipzig. (ESPN)
Kiungo wa Liverpool, Jordan Henderson, 33, na mshambuliaji wa Chelsea, Pierre Aubameyang, 34, wapo kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na Ettifaq baada ya klabu hiyo kumteua Steven Gerrard kuwa kocha mkuu. (Mail)
PSG inapanga kuivuruga Chelsea, Liverpool na Manchester City katika usajili wa kiungo raia wa Hispania, Gabri Veiga, 21, kutoka Celta Vigo. (The Guardian)
Liverpool imepiga hatua kadhaa katika mbio za kumsajili kiungo Romeo Lavia wakati huohuo imeripotiwa klabu hiyo inapanga kuwasilisha ofa yao ya kwanza. Southampton wanataka £50m. (Talksport).
Arsenal iko tayari kufanya usajili wa kiungo Lavia kutoka Soton, watakamilisha dili hilo mara baada ya kumalisha usajili wa Declan Rice. (Times – subscription required).
Man United inakaribia kumpa mkataba mpya mshambuliaji Marcus Rashford, wakati huohuo wanaendelea na mipango ya kumnasa mshambuliaji Randal Kolo Muani, 24.
(CBS)