Tetesi za usajili Ulaya

STRAIKA wa Spurs,Harry Kane hataki kujiunga na PSG msimu huu na Mwingereza huyo anyehusishwa na Bayern Munchen ameripotiwa kuwa hataki ofa yoyote kutoka timu hiyo. (Telegraph)

Kuna uwezekano Totenham Spurs ikafanya usajili wa mshambuliaji Ivan Toney kutoka Brentford. Toney kwa sasa atatumikia adhabu ya kufungiwa mpaka Januari. Uhamisho huo utategemea mustakabali wa Harry Kane. ( Foot ball transfer)

Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi amepanga kuonana na Kylian Mbappe kwa mara ya kwanza tangu mchezaji huyo alipotuma barua kwenye klabu hiyo kuwa hataongeza mkataba. (Sky Sport)

Chelsea imepanga kuongeza dau mpaka £70m kwa ajili ya kumnasa kiungo Moise Caicedo kutoka Brighton. ( Standard)

West Ham United imeingilia kati mpango wa Man United kutaka kumsajili kiungo Leon Goretzka kutoka Bayern Munchen. (Sky Germany)

Habari Zifananazo

Back to top button