TETESI ZA USAJILI ULAYA

HABARI za wakati huu mdau wa michezo, popote pale unapotufuatilia kupitia mitandao yetu, ikiwa ni Januari 2, 2023 karibu sana tukupitishe katika tetesi za usajili barani Ulaya huku dirisha la usajili likiwa limefunguliwa.

Miongoni mwa yale utakayoyasoma mchana huu ni kuhusiana na usajili wa Arsenal, Manchester United huku Chelsea ikikaribia kukamilisha usajili wa mchezaji kutoka Monaco ya Ufaransa.

FRANKEI DE JONG

Advertisement

Kiungo wa Barcelona, Frankie De Jong amebadili maamuzi yake na sasa anataka kujiunga na Manchester United. Hii kwa mujibu wa mtandao wa Fichajes wa nchini Hispania.

BENOIT BADIASHILE

Taarifa zinaeleza kuwa Chelsea huenda ikamtangaza nyota wa Monaco, Benoit Badiashile, 21, kuwa mchezaji wao baada ya taarifa ya Skysport kueleza kuwa mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya leo.

DENZEL DUMFRIES

Taarifa inayoendelea kuumiza vichwa vya watu wengi ni kuhusu usajili wa beki raia wa Uholanzi, Denzel Dumfries anayehusishwa kujiunga na Chelsea na Manchester United, taarifa ya mtandao wa Marco Barzaghi imeeleza timu hizo zinapigana vikumbo kupata saini ya beki huyo wa Inter Milan.

MYKHAILO MUDRYK

Mtandao wa Sport Arena wa Ukraine umeeleza kuwa Arsenal wamefikia makubaliano binafsi ya mkataba wa miaka mitano wa kumsajili kiungo Mykhailo Mudryk, 21 kutoka Shaktar Donetsk.

ENZO

Imeelezwa kuwa Chelsea bado haijakata tamaa na inaendelea kusukuma uwezekano wa kumnasa kiungo mkabaji wa Benfica, Enzo Fernandez  (Metro).

YOURI TIELEMANS

‘The Express’ kutoka Uingereza imeeleza kuwa Arsenal inaweza kumnasa, Youri Tielemans kutoka Leicester City, baada ya timu hiyo kuanza mazungumzo na Angers ya Ufaransa juu ya usajili wa Mmoroco, Azzedine Ounahi, 22, kuziba pengo hilo.

BUKAYO SAKA

Arsenal wameanzisha kipengele cha kuongeza mkataba wa winga wa Uingereza Bukayo Saka kwa mwaka mmoja huku wakijadili mkataba mrefu zaidi na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

/* */