SHIRIKISHO la soka nchini TFF limesogeza mbele mchezo wa nusu fainali ya ASFC kati ya Yanga dhidi ya Singida Big Stars mpaka utakapopangiwa tarehe nyingine.
Mchezo huo ulipagwa kuchezwa Mei 7, katika Uwanja wa Liti Singida.
Katika taarifa yao iliyotolewa leo Mei 2, 2023 TFF imeeleza kuwa mchezo mwingine kati ya Simba SC na Azam FC ambao ulipangwa kuchezwa Jumamosi Mei 6, sasa utapigwa Mei 7, 2023 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara.
TFF imesema kuwa mabadiliko hayo yametokana na maombi ya Yanga ya kutaka kubadilishiwa muda wa mchezo huo, ili kupata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants utakaochezwa Mei 10, 2023 Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.