TFF yasaini mkataba na Precision Air

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh milioni 108 na Shirika la Ndege la Precision Air katika kushughulikia suala la usafiri wa anga.

Akizungumza leo Novemba 2, 2022, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema kuwa shirika hilo limekuwa msaada kwenye mpira wa miguu kwa kusafirisha timu mbalimbali wakiwemo wenyewe TFF.

”Precission wameingia nawaambia hawatatamani kutoka kwa sababu ya nguvu ya mpira kama ilivyo kwa wale ambao tayari wameingia,” amesema Karia.

Amesema licha ya kuwa na mikataba mbalimbali, ila mkataba na shirika hilo umekuwa wa kihistoria ukiwa ni mkataba wa kwanza wa usafirishaji wa anga.

Mkurugenzi wa Precision Air, Patrick Mwanri ameisifu TFF kwa hatua waliyopiga katika soka na kwamba suala hilo limewavutia kufanya kazi pamoja na kuongeza kuwa ushirikiano huo utaongeza nguvu katika soka.

”Precision Air itadhamini kombe la Azam Sports Federation kwa msimu wa 2022/2023 kwa kutoa tiketi zenye thamani ya Sh milioni 108 kwa msimu wa 2022/23,” Patrick Mwanri.

Habari Zifananazo

Back to top button