TFS, wadau mazao ya misitu wateta

ARUSHA: WAVUNAJI wa mazao ya misitu wametakiwa kuvuna maeneo yao waliyopewa ili kuiwezesha serikali kupata mapato.

Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS ) Profesa Dos Santos Silayo, Kaimu Kamanda wa Kanda ya Mashariki  Mathew Ntilicha, amesema hayo kwenye kikao cha Wadau wa misitu Kanda ya Mashariki na Kaskazini

“Sisi tuna jukumu la kukaa na wadau na kuwaelekeza na kusaidia sehemu yenye changamoto.

“Tunapenda sana unapokuwa umepewa uvunaji, kama mvunaji ujitahidi uvune, usipovuna yale malengo yaliyowekwa na serikali hatutaweza kuyafikia,” amesema.

Amesema TFS umeona ufanye kikao na wadau wa mazao ya misitu Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.

Vile vile na Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Amesema lengo ni kujadili mustakabali wa kuendelea kuboresha kazi zinazofanywa kila siku na wakala huo.

Habari Zifananazo

Back to top button