TGNP wazungumzia bajeti 2024/25

DAR ES SALAAM; Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa jinsia nchini(TGNP) ,Gemma Akilimali, amesema ili bajeti ya Serikali mwaka 2024/2025 ikidhi matakwa ya Watanzania inatakiwa ishirikishe makundi yote.

Akilimali amesema hayo  mapema leo jijini Dar es Salaam, wakati akitoa maoni juu ya bajeti ya mwaka 2024/2025 inayotajiwa kuwasilishwa leo jioni bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba.

Amesema kumekuwa na changamoto kuhusu bajeti zinazowasilishwa zimekuwa hazikidhimatakwa ya makundi yote.

“Upungufu ambao tunaona ni ushikirishwaji kutoka chini na jinsi gani wananchi wanapewa kipaumbele,”amesema Akilimali, ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake nchini.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi, amesema ni vyema bajeti  ijikite pia katika kutatua changamoto ya vifo vya mama na watoto.

 

Habari Zifananazo

Back to top button