Thamani biashara Tanzania, Kenya ipo juu

KENYA; Nairobi. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amesema thamani ya biashara kati ya Tanzania na Kenya kwa mwaka 2022 ilifikia Sh trilioni 1.8.
Akihutubia leo Desemba 12, 2023 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kenya kwa niaba ya Rais Samia, Dk Mwinyi amesema Kenya pia ni miongoni mwa nchi 10 zinazoongoza kwa uwekezaji Tanzania.
“Kutokana na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo, nchi zetu mbili zimeweza pia kunufaika kiuchumi, hususan katika nyanja za biashara na uwekezaji.
“Mathalan, thamani ya biashara kati ya nchi zetu kwa mwaka 2022 ilifikia shilingi trilioni 1.8, sawa na takriban Dola za Marekani milioni 800. Kenya pia ni miongoni mwa 10 zinazoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania. Hii inaonesha kuwa Kenya ni mshirika na mbia wetu muhimu wa maendeleo,” amesema Dk Mwinyi.
1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *