Theresa May kuachia ubunge

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kuwa atajiuzulu kama mbunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Katika taarifa yake kiongozi huyo alisema amechukua uamuzi huo mgumu wa kujiondoa bungeni baada ya miaka 27.

May ,67, pia aliahidi kuunga mkono serikali ya Rishi Sunak na kusema anaamini kuwa chama cha Conservatives kinaweza kushinda uchaguzi ujao.

May ambaye amechagulia mara saba, amekuwa mbunge wa Conservative katika jimbo la Berkshire tangu 1997.

Kiongozi huyo alihudumu kama Waziri Mkuu kuanzia 2016 hadi 2019, akiwa ameshikilia wadhifa wa katibu wa ndani tangu 2010. May aliingia ‘Downing Street’ baada ya David Cameron kujiuzulu kufutia nchi hiyo kupiga kura ya kujiondoa Umoja wa Ulaya jambo ambalo alipinga.

Habari Zifananazo

Back to top button