Thiago Silva nje wiki sita
KOCHA wa Chelsea, Graham Potter amesema beki Thiago Silva atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo wa EPL dhidi ya Tottenham Hotspurs Februari 26, 2023.
Silva aliumia wakati akikabana na mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane dakika ya 17 ya mchezo huo ulioisha kwa Chelsea kupoteza mabao 2-0.
Potter ametoa taarifa njema za kurejea kwa kiungo Ng’olo Kante ambapo alisema “amekuwa na mazoezi leo ila bado anahitaji muda kurejea”.
Kuhusu kipa Eduardy Mendy, Potter amesema anaendelea vizuri ila bado hajapona vizuri.