TID adai kuteka mashabiki

Khalid Mohamed ‘TID’

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ ametamba kuwa siri kubwa ya kukubalika kwake na mashabiki ni uwezo aliokuwa nao wa kuimba na kulitawala jukwaa.

Akizungumza na HabariLEO, msanii huyo alisema wasanii wengi pamoja na uwezo mkubwa waliokuwa nao katika kuimba lakini hawawezi kulitawala jukwaa vizuri.

“Naweza kusema mimi ndio mburudishaji halisi sababu sauti yangu tungo zangu zinavutia mashabiki waliopo ukumbini lakini nina uwezo mkubwa wa kulitawala jukwaa jambo ambalo wasanii wengi hawana,” alisema TID.

Advertisement

Alisema tangu ameanza muziki wa ushindani mwanzoni mwa mwaka 2000, alikuwa ni mtu anayependa kucheza na amekuwa akiwafuatilia kwa karibu wasanii wa nje ndio maana amekuwa bora katika nafasi hiyo.

Alisema pamoja na ukongwe wake kwenye muziki huo lakini bado hajaona msanii ambaye anamfikia katika kutawala jukwaa na hiyo ndio silaha yake kubwa sababu ni jambo ambalo analipenda na analifanyia mazoezi kila siku.