Kamati kutathmini hali vyombo vya habari yaundwa

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameunda kamati ya watu tisa ya kutathmini vyombo vya habari na maslai ya wanadishi.

Kamati hiyo inaongozwa na Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando ambaye ndio Mwenyekiti huku Katibu akiwa Msemaji wa serikali Gryson Msigwa.

Wajumbe ni Rose Reuben Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa), Joyce Mhavile Mkurugenzi Mtendaji wa ITV, |Sebastin Maganga, Mkuu wa Maudhui Clouds Media Group, Bakari Machumu, Mkurugenzi Mtendaji Mwananchi Communication, Keneth Simbaya Mkurugenzi Umoja wa Club za Waandishi wa Habari nchini (UTPC) Jacquline Owiso kutoka DSTV na Mpiga picha mkongwe Richard Mwaikenda.

Advertisement

Akizungumza mara baada ya kutangaza kamati hiyo, Nape amesema ameunda kamati hiy9o ili kutathmini hali ya uchumi katika vyombo vya Habari ambapo kamati hiyo itafanya kazi kwa miezi mitatu.

“Ndani ya miezi mitatu iwe imemaliza kazi yake, jukumu kubwa ambalo kamati hi itafanya ni kupata taarifa ya hali vya vyombo vya Habari kiuchumi na kiutendaji, taarifa ipatikane tuone namna ya kuchakata kukwamua tasnia ya Habari, ” amesema Nape na kuongeza:

“Kamati itafanya kazi ya kupata taarifa ya hali ya waandishi wa Habari katika vyombo vya Habari wakiwemo walioajiriwa, wenye mikataba, wawakilishi mikoani na wengine wanaoshirikiana na vyombo vyetu katika kazi ya habari, tunataka watuletee hali ya mikataba inavyoheshimiwa, tunataka kulinda maslahi ya waandishi.” amesema.

Nape amewataka waandishi kutoa ushirikiano unaohitajika kwa kamati wakati wa kuchakata taarifa kwa kutoa maoni yao ipasavyo.

“Bahati nzuri, mchakato wa mwisho wa mabadiliko ya sheria ya Habari, kama Wizara tumeshakamilisha, na kuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa utaratribu wa kupeleka bungeni,” amesema.