Tigo, Samsung wafanya jambo magulio ya simu

MAGULIO ya simu yametoa ahuweni kwa wananchi ambao wamenunua simu kwa kulipia kidogo kdiogo kupitia program maalum iliyowekwa na Samsung kwa kushirikiana na Tigo.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari inasema kuwa kupitia program hiyo wateja wataweza kuchagua kati ya simu aina ya A04 na A04s na kulipa kuanzia Sh 1,000 kila siku kwa muda wa mwaka mmoja.

Taarifa hiyo inasema kuwa magulio hayo yameandaliwa na kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na Samsung kuanzia Aprili 17 jijini Dar es Salaam na Mwanza.

“Gulia hili pia litazinduliwa Kibo Complex-Tegeta Mei 4. Magulio hayo yatakamilika Mei 14, 2023 ili kuwapa wateja mwezi mzima wa kufanya manunuzi ya simu za Samsung na kufurahia zawadi zenye kusisimua na vufurushi, “imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema pamoja na kupata unafuu wa kulipia simu hizo, wateja pia watapata uzoefu wa simu mpya za Samsung Galaxy S23 (S23 Ultra; S23 Plus na S23) pamoja na toleo jipya la A series (A34 na A 54 5G)

“Wateja watakaonunua simu mpya za A series (A34 na A54) wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo chupa za kishua, ‘coffee mugs’ na tisheti. Promosheni hii ya nunua ushinde itaanza wakati wa wiki ya Eid na itahusisha pia maduka mengine ya Samsung, “imesema taarifa hiyo

Taarifa hiyo imesema kuwa simu hizo zina kamera bomba yenye pixel ya hali ya juu yenye uwezo mzuri wa kuchukua video na picha zinazong’aa na zenye mvuto. Pia zina betri imara zenye uwezo wa kudumu na chaji kwa siku mbili mfulululizo.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button