Tigo yajivunia mikopo kwa wakulima
KAMPUNI ya Tigo inayosaidia kuleta mageuzi ya kidijitali nchini, leo imezindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja huku ikijivunia jinsi mpango wake wa kukopesha simu janja kwa wakulima, unavyochochea mageuzi na kuongeza tija katika sekta hiyo.
“Katika kanda yetu mpango huu umewanufaisha sana wakulima wakiwemo wale wa korosho, ufuta, chai na kokoa na kuchochea maendeleo yao,” alisema Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Abbas Abdulrahaman.
Alisema kampuni yao imetenga fungu maalumu kuwawezesha wakulima kupaya mikopo ya simu za kisasa kwa kuwa inatambua matumizi ya simu yanawawezesha kupata taarifa za hali ya hewa, mbinu za kilimo, bei za pembejeo na bidhaa moja kwa moja kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika.
“Lakini pia simu zinaweza kuwasaidia wakulima kutafuta masoko ya mazao, kujua beo za soko na hata kufanya biashara moja kwa moja kutoka shambani,” Abdulrahman alisema.
Katika kuboresha mawasiliano ya mtandao wao wa simu alisema Tigo ipo katika utekelezaji wa mpango unaolenga wateja wao nchini kote kupata mawasilino kupitia teknolojia ya 4G na baadhi ya maeneo kwa kupitia 5G.
Awali Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Mwangaza Matotola alisema
Tigo inatambua mchango wa watoa huduma wake katika kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye ubora.
Matotola alisema huduma kwa wateja ni kitovu cha biashara yao na ndiyo maana wameweka kipaumbele katika kuhakikisha inatolewa kwa ubora na weledi siku zote ili kukidhi mahitaji ya wateja wao.
“Tigo imeendelea kuwekeza katika kuboresha huduma kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wetu na zaidi tumewekeza zaidi katika kujenga miundombinu ya mawasiliano ili kuhakiisha wateja wanapata huduma za uhakika,” alisema