BEKI Jullien Timber atarejea uwanjani kabla ya kumalizika kwa msimu huu, meneja wa Arsenal, Mikel Arteta ameeleza leo.
Timber alimuia katika mchezo wa ufunguzi wa ligi wa Ngao ya Hisani dhidi ya Manchester City mwezi Agosti mwaka jana.
Akizungumza kuelekea mchezo wa EPL kesho dhidi ya Newcastle United, Arteta amesema: “Amekuwa karibu na wachezaji wengine uwanjani na ataanza kufanya mazoezi nasi wiki ijayo au zaidi”.
Akizungumzia kurejea kwa kiungo Thomas Partey amesema: “Ngoja tuone tuna mazoezi mengine wazi hatukuwa naye miezi mingi. Sawa na Gabby, amefanya mazoezi kiasi, Alex hayuko mbali. Tomiyasu bado kidogo.”