Timu 12 kunogesha mapinduzi Cup 2024

Z’BAR: TIMU 12 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kushiriki kombe la Mapinduzi kuanzia Disemba 28, 2023 hadi Januari 13 mwakani.

Akitoa taarifa ya kamati ya Kombe la Mapinduzi kwa waandishi wa habari, Forodhani, mjini Unguja, Makamu Mweyekiti wa Kamati ya kombe la Mapinduzi, Suleiman Jabir amesema maandalizi ya kombe hilo tayari yamekamilika ambapo pazia la ligi hiyo linatarajiwa kufunguliwa mwezi huu.

Advertisement

Amezitaja timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na Mlandege, KVZ, Jamuhuri na Chipukizi kwa upande wa Zanzibar na timu ya Azam, Simba, Singida Fountain Gate na Yanga kutoka Tanzania Bara.

Ameongeza kuwa katika kuendeleza ujirani mwema wa kimichezo wamezialika Timu ya URA kutoka Uganda, Bandari kutoka Kenya na APR ya Rwanda.

Amesema mashindano hayo yatachezwa katika Uwanja wa Amani, hivyo wananchi watarajie michuano yenye mvuto kulingana na ubora wa uwanja huo.

Makamu Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) amempongeza Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi kwa uboreshaji wa miundombinu ya Michezo kwa kujenga viwanja vya kisasa ambavyo vitawasaidia Vijana wa Zanzibar kuendeleza vipaji vyao.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni timu ya Mlandege iliyotwaa ubingwa huo baada ya kushinda magoli 2 -1 dhidi ya Singida Big Stars, ikiwa wote ni fainali yao ya kwanza ya kombe hilo ambalo ni maalumu kwaajili ya kuazimisha Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *