TIMU nane zilizofanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali zimekabidhiwa jezi katika mashindano ya soka ya Mega FM Super Cup yaliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Arusha (ADFA).
Timu hizo nane ni Suye, Lengo, Morombo, Kimandolu, Arusha City, Old Boys, Nyota na New Hope zimetinga hatua hiyo katika mashindano hayo yanayotarajiwa kumalizika Julai 23, mwaka huu .
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Katibu wa ADFA Fredrick Lymo, amesema mashindano hayo yamefika hatua ya robo fainali na changamoto zote zikiwemo za viwanja na waamuzi zinafanyiwa kazi, ili mpira uweze kuchezwa kwa ushindani zaidi.
Naye Meneja wa Mega FM, Amani James ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo, wataendelea kutoa ushirikiano kwa ADFA katika juhudi za kuendeleza mpira.
Bingwa katika mashindano hayo atazawadiwa Sh milioni moja, mshindi wa pili Sh 500,000, huku pia kukiwa na zawadi kwa Mchezaji Bora, Kipa Bora na Kocha Bora.
Comments are closed.