Timu za JKT zapewa mbinu

DAR ES SALAAM: Wachezaji wa timu za mpira wa miguu za JKT wametakiwa kuwa na upendo umoja na mshikamano na wajue kinachohitajika ni ushindi katika kulisakata kabumbu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania Jenerali, Jacob Mkunda wakati anakabidhi magari matatu kwa timu za jeshi ambazo ni JKT Tanzania, JKT Queens na Mashujaa FC ambayo yanauwezo wa kubeba watu 56 kwa wakati mmoja.

“Nipende kuwasisitizia upendo na mshikamano mjue ninyi ni ndugu lakini sio sababu ya kuachiana magoli kila mtu acheze kwa bidii lakini acheni chuki za hapa na pale baada ya mechi ninyi ni watoto wa baba mmoja chezeni kwa weledi.”

“Michezo ni afya, ajira na huleta mshikamano katika  taifa ni sehemu ya kuwakutanisha watu kuweza kuongea lugha moja kupitia michezo.”

Pia Jenerali Mkunda amezindua kamati ya uanzishwaji wa vituo vya michezo ambapo amesema kuwa vituo hivyo vitasaidia kuinua na kuendeleza vipaji vya vijana kucheza michezo mbalimbali.

“Gari zipo za timu zote za JKT leo nazindua tatu mmoja ipo bandarini nayo ni miongoni mwa gari za usafiri za wachezaji wa timu hizo.”

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF Wallace Karia, amempongeza mkuu wa majeshi kwa kutoa magari kwa wachezaji wa timu za JKT Qeens, JKT Tanzania, Mashujaa FC na magari manne.

Habari Zifananazo

Back to top button