Tina Tuner afariki Dunia

MALKIA wa Rock ‘n’ Roll’ duniani Tina Turner amefariki dunia Mei 24,2023 akiwa na umri wa miaka 83.

Mkongwe huyo wa muziki duniani, amefariki huko Kusbacht, Zurich Uswizi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Nyota huyo mzaliwa wa Marekani alikuwa mmoja wa waimbaji mahiri wa rock, na alitamba na vibao vyake vya The Best, Proud Mary, Private Dancer na What’s Love Got to Do With It.

Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa heshima zao za mwisho ni wanamuziki Sir Mick Jagger, Sir Elton John, Diana Ross, Bette Midler na Giorgio Arman

Habari Zifananazo

Back to top button