TUME ya Uchaguzi nchini Nigeria (INEC) imeamtangaza Bola Tinubu kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais katika uchaguzi uliokumbwa na utata, huku viongozi wa upinzani wakipinga uchaguzi huo kuwa uligubikwa na utata na kutaka urudiwe mpya.
Tinubu, 70, anawakilisha chama tawala cha All Progressives Congress, ambacho kilipata karibu kura milioni 8.8 – takriban 36.6% ya kura zote, hiyo kwa mujibu wa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Mahmood Yakubu.
Rais huyo mteule alimshinda makamu wa rais Atiku Abubakar wa chama cha upinzani cha People’s Democratic Party (PDP), na mgombea maarufu wa kikosi cha tatu Peter Obi, ambaye amepata umaarufu miongoni mwa vijana hasa. Katika hotuba ya kukubalika kwake.
Chama cha upinzani cha PDP kimeyaapuuza matokeo ya uchaguzi huo na kudai uchaguzi mpya kutokana na kile wanachodai kuwa kuwekuwa na wizi mkubwa wa kura.
Uchaguzi huu ni miongoni mwa chaguzi zenye upinzani mkali tangu nchi hiyo irejee kwenye utawala wa kidemokrasia mwaka 1999, huku zaidi ya watu milioni 93 wakiwa wamejiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa INEC.
Aidha Tinubu aliwashukuru wapiga kura na kusema “amenyenyekea sana.” “Huu ni wakati mzuri katika maisha ya mwanadamu yeyote na uthibitisho wa uwepo wetu wa kidemokrasia,” alisema. “Nawakilisha ahadi na kwa msaada wako, najua ahadi hiyo itatekelezwa.” Pia akiwaomba “waungane pamoja” ili kuimarisha nchi.