Tinubu kuapishwa rasmi leo

Gavana wa zamani wa Lagos, Bola Ahmed Tinubu, , anatarajiwa kuapishwa leo kuwa rais mpya wa Nigeria.

Bola Tinubu, 71, alishinda uchaguzi wa Februari kwa ahadi ya kurejesha matumaini  lakini anakabiliwa na changamoto ngumu za kiuchumi na kiusalama.

Atamrithi  Rais wa mihula miwili Muhammadu Buhari,80, huku nchi ikiwa  na mfumuko wa  juu wa bei, viwango vya juu vya deni la Taifa  na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara.

Ushindi wa Bw Tinubu unapingwa na upinzani mahakamani kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata mwezi Februari.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa , Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ni miongoni mwa viongozi waliowasili katika hafla ya kuapishwa katika mji mkuu Abuja.

Wengine ni Rais wa Jamhuri ya Kongo-Brazzaville, Denis Sassou Nguesso, rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embaló na Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, Rais wa mpito wa Chad Mahamat Déby, Rais wa Jamhuri ya Niger, Mohamed Bazoum na Rais Nana Akufo-Ado wa Ghana.

Bw Tinubu anaweza kuwa na muda mchache wa kusherehekea. Wananchi wa Nigeria wanatarajia hatua za haraka.

Mfumuko wa bei unaendelea kwa kiwango cha juu zaidi kwa karibu miaka 18, mtu mmoja kati ya watatu hawana ajira na pato la sekta muhimu ya mafuta linapungua.

Itabidi achukue hatua za haraka ili kuwaaminisha watu ambao hawakumpigia kura kwamba yuko tayari kutekeleza majukumu yake.

Habari Zifananazo

Back to top button