TIRA kuanzisha skimu bima ya kilimo

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ipo mbioni kuanzisha skimu ya Bima ya Kilimo kwa ajili ya utoaji majibu ya changamoto zinazowakabili wakulima hususani kwenye mabadaliko ya hali ya hewa kwakushirikiana na Wizara ya Kilimo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Taifa ya Bima, Kamishna wa Bima, Dk,Baghayo Saqware amesema bima hiyo itawasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi sanjari na kupata taarifa mbalimbali za kilimo, mabadaliko ya hali ya hewa na tabia nchi kwalengo la kuwapa Kinga wakulima wadogo nchini

Pia uwepo wa mifumo ya Tehama umewezesha Mamlaka hiyo kutoa leseni kwa muda mfupi ikiwemo utoaji wa mafunzo kuhusu bima kwa viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Tanzania ikiwemo uwepo wa mabalozi wa bima wanaotoa elimu ya bima kwa watumishi na watu mbalimbali.

“Bima hii itasaidia sana wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo ili waweze kupata mazao yao na kujikwamua kiuchumi”

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x