TIRA kusimamia madai na fidia kulipwa kwa wakati

DAR ES SALAAM: Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imesema itaendelea na mkakati wake wa utoaji elimu kwa Umma kwa kushirikisha wadau wote ili kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2030.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Bima Tanzania, Dk.Bakayo Saqware wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kupitia mkutano ulioandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina Jijini Dar Es Salam.
Amesema mamlaka itaendelea kusimamia kampuni zote za Bima kuhakikisha zinalipa madai na fidia kwa wakati kwa wateja wao wanapopata matatizo ambapo hadi sasa ulipaji wa madai na stahiki umefikia asilimia 95 hivyo kumepunguza malalamiko kwa wateja.
Akizungumzia matarajio yao hadi ifikapo mwaka 2026, Kamishna amesema ni pamoja na kuanza kutekeleza mpango wa kitaifa wa bima ya kilimo pamoja na uanzishwaji wa bodi ya wataalamu wa Bima hifadhi ya jamii na kuweka takwimu za Bima.
Akizungumza kwa niaba ya Wahariri Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deudatus Balile ameishauri Mamlaka kuweka mpango utakaosaidia kumaliza changamoto katika utendaji kazi wake.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button