TIRA yatoa maelekezo fidia katika majanga

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imewataka wananchi kutumia namba ya maajabu ya kuhakikisha gari analosafiria kama lina bima ndipo apande ili yanapotokea majanga aweze kufuatilia fidia.

Kamishna wa TIRA, Dk Baghayo Sakware amesema hayo leo Dar es Saalam wakati mamlaka hiyo ikisaini hati ya makubaliano na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri nchi Kavu (LATRA).

Kuhusu namba ya maajabu ameitaja kuwa ni *152*02# na kufuata maelekezo ya namna ya kuhakiki gari kabla ya abiria kupanda. chombo chochote cha usafiri,jambo litakalomuwezesha kujua kama gari limekatiwa bima ama laa.

Amesema ni mfumo unaorahisisha abiria kujua kwamba anaweza kufidiwa pindi gari lipatapo tatizo hivyo kama gari halijakatiwa bima asipande.

Kuhusu hati ya makubaliano amesema kwa sasa kampuni za bima zinaweza kutoa leseni na itarahisisha pia kutoa fidia Kwa wahanga na kurahisisha uhakiki kama wasafirishaji Wana bima.

Amesema makubaliano yanaanza mwaka huu na kwamba yatasaiia kuondoa vikwazo na kuongeza ufanisi .
“Tunakwenda kushirikiana kutoa elimu kwa umma, kutoa taarifa za chombo cha moto kinavyotakiwa kufuata taratibu,”amesema Dk Sakware na kuongeza kuwa watoa huduma za bima nchini watasaiidia kutoa huduma.

Kwa upande wake Suluo amesema watanzania wengi hawana elimu ya kwamba anaweza kufidiwaje iwapo atapata ajali na kuumia na kwamba ni wapi anapoweza kwenda kusaidiwa.

Amesema kwa makubaliano hayo Wakala wa bima anaweza kutoa leseni na kutoa elimu pia kuhusu bima lengo likiwa kuwahudumia wananchi kwa karibu.

Amesema upo usumbufu na mlolongo wa ufuatiliaji wa fidia ambapo elimu inatakiwa kutolewa kwamba mlalamikaji anatakiwa kutunza risiti za magari na hata za hospitali Ili zitakapohitajika aweze kufidiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button