TLS kumtetea mjane wa nyama ya swala

CHAMA cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kanda ya Iringa wameanzisha mchakato wa kumsaidia kisheria mjane Maria Emirio Ngoda aliyehukumiwa na Mahakama ya Mkoa wa Iringa kifungo cha miaka 22 kwa kosa la kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha pasipo na shaka kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000.

Kwa kupitia taarifa yao waliyoitoa mapema leo, Mwenyekiti wa TLS kanda ya Iringa, Wakili Moses Ambindwile pamoja na Wakili Cosmas Kishamawe wamesema kwa kushirikiana na mawakili wengine wa mkoani Iringa tayari wameanzisha mchakato wa kumsaidia kisheria mjane huyo.

Mawakili hao wamesema tayari mchakato wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Mkoa wa Iringa umeanza rasmi leo asubuhi ikiwa ni muendelezo wa mpango wao wa kutoa msaada wa ushauri na utetezi wa kisheria kwa makundi mbalimbali ya kijamii yasio na uwezo.

Ambindwile alisema toka waanzishe mpango wa kutoa msaada wa ushauri wa kisheria mkoani Iringa wameendelea kupokea maombi kutoka kwa makundi ya watu wasio na uwezo kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.

“Tuishukuru sana kampuni ya Asas kwa ahadi yake iliyotolewa na mmoja wa wakurugenzi wake Ahamed Asas kwa kujitokeza kushirikiana nasi ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi wasio na uwezo hususani wale waishio vijijini,” alisema.

Akitoa hukumu hiyo kwa mjane huyo mkazi wa Zizi la Ng’ombe mjini Iringa, Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, Mkasiwa alisema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 86 (1) (2) (c) cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba tano ya mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho na kifungu cha 59 (a) (b) cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2016.

Wakati akijitetea bila usaidizi wa wakili yoyote, mjane huyo alikiri ni kweli alikutwa na ndoo yenye nyama hiyo ambayo alidai alikabidhiwa na mtu aliyemtambua kwa jina moja la Fute bila kujua ina nyama ya nini ndani yake.

Licha ya kumtaja na kumtambua Fute alisema alilazimishwa abebe ndoo hiyo na kufikishwa kituoni na kufunguliwa kesi ya kukutwa na nyara za serikali sambamba na kosa la uhujumu uchumi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kana ushamba
Kana ushamba
26 days ago

HONGERA TBC, TBA, TBS, TIB BANK, DTB, TBL, MTB MNAFANYA NCHI INANYOOKA VYEMA..

Kana ushamba
Kana ushamba
26 days ago

HONGERA TBC, TBA, TBS, TTB, TIB BANK, DTB, TBL, MTB MNAFANYA NCHI INANYOOKA VYEMA..

Paul Henry
Paul Henry
25 days ago

Yani kweli kabisa nyie mkamfunge mjane wa watu kwa kosa la nyama wakati nyie mliuza twiga na bandari na bado mnatuibia. Mungu awaone

Angila
Angila
25 days ago

I have just received my 3rd paycheck which said that $16285 that i have made just in one month by working online over my laptop. This job is amazing and its regular earnings are much better than my regular office job. Join this job now and start making money online easily by
.
.
.
.
Just Use This Link……..> > > http://Www.Smartcareer1.com

Zairo Ismail
Zairo Ismail
24 days ago

Sheria kali na adhabu kali kwa watu wanyonge

James Stanley
James Stanley
23 days ago

Serikal acheni kunyanyasa watu

Back to top button
6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x