MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadharisha juu ya uwepo wa upepo mkali kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia leo katika mikoa ya Lindi, Tanga, Mtwara, Pwani na Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari jana, upepo huo mkali utafikia kasi ya kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa tahadhari hiyo imetolewa kwa maeneo ya ukanda wa Pwani ambayo ni Lindi, Tanga, Mtwara, Pwani na Dar es Salaam, yakijumuishwa pia maeneo ya visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa TMA upepo huo unatabiriwa kuvuma kuanzia leo na keshokutwa na Ijumaa hakuna tahadhari yoyote.
Ilibainisha kuwa inatabiriwa upepo huo unaweza kuwa wa wastani au kiwango cha athari.