MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa katika mikoa 11 kwa siku tatu, hivyo kuwataka wananchi kuwa makini nazo.
Taarifa iliyotolewa jana na TMA ilitoa angalizo hilo la mvua kubwa katika maeneo machache ya mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Kusini mwa mkoa wa Morogoro, Mbeya, Songwe, Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara.
Ilieleza kuwa uwezekano wa kutokea kwa angalizo hilo kuanzia jana mpaka Jumatano ni kwa kiwango cha wastani.
Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za uchumi na usafirishaji.