TMDA: Hakuna dawa ya kuongeza makalio, matiti

IRINGA; USIDANGANYIKE na matangazo kuwa unaweza kupata dawa za kuongeza unene wa makalio, matiti au kiungo kingine chochote cha mwili!

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema hakuna dawa hiyo yenye uwezo huo wa kuongeza kiungo chochote cha mwili.

Akizungumza katika kikao kazi katI ya TMDA na wahariri wa habari kilichofanyika Mei 16, 2024 mjini Iringa, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dk Adam Fimbo, amehadharisha jamii juu ya upotoshaji huo unaofanyika kupitia matangazo hususani kwenye mitandao ya kijamii.

“TMDA hatuna dawa yoyote tuliyoletewa na tukaifanyika uchunguzi ya kukuza makalio, matiti wala kukuza viungo kwa binadamu…Ukitaka labda kufanya hayo ili kuona mabadiliko labda ufanye upasuaji,” amesema Dk Fimbo.

Amesema TMDA inatambua mchango wa vyombo vya habari katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu shughuli za udhibiti wanazofanya.

Habari Zifananazo

Back to top button