TMDA yaeleza madhara dawa zilizoisha muda

MAMLAKA ya Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) imeainisha madhara ya kutumia dawa zilizoisha muda wake ikiwa ni pamoja na dawa hizo kushindwa kutibu madhara yaliyokusudiwa na mtumiaji.

Akizungumza wakati wa Mahojiano na HabaraiLEO ,Meneja Mawasiliano wa TMDA ,Gaudensia Simwanza amesema dawa zilizoisha muda wake lengo la matumizi yake inaweza lisitimie na wakati mwingine kusababisha madhara mengine.

“Madhara ya kutumia dawa ambazo zimeisha muda wake kwanza mtu anatumia dawa ili apone hivyo anapotumia hiyo dawa inatashindwa kupona kutokana na dawa hizo kutokuwa na nguvu.

Simwanza amesema utumiaji wa dawa hizo unamaanisha kuwa Muhusika anatumia kitu ambacho hakuna anayejua ubora wala usalama wake na wanaweza kusema ni sumu kwani hakuna ufanisi.

Amebainisha kuwa ili kuthibitisha kuwa dawa inafaa kwa matumizi lazima kwanza imefanyiwa majaribio,imepimwa itakaa uhai muda gani na baada ya muda huo haitakuwa na nguvu kwani inapimwa uwezo wa kutibu kuwa itafanya kazi muda gani.

Simwanza amesema dawa zote zinafanyiwa majaribio ya kisanyasi na tafiti hivyo mtu haibuki tu na kusema dawa hii itakaa muda fulani ndo maana usajili wa dawa unachukua muda mrefu kuangalia hivyo vitu vyote.

“Kama wamesema inakaa muda wa miaka mitatu tunaangalia je ndani ya hiyo miaka mitatu itaweza kutibu ? ndo maana tunasema mtumiaji atumie kitu ambacho kipo ndani ya huo muda ,”ameeleza.

Aidha ameanisha kuwa biashara ya dawa ni tofauti na ndio maana wanaotaka kuuza dawa wanatakiwa kusomea kada ya afya na kwamba humo kuna maadili ambapo licha ya kusoma wanaongozwa na maadili na ndio maana wanaapa kabla ya kufanya kazi na baraza la famasia wanasimamia maadili yao.

“Sisi TMDA tunachofanya kwanza tunatoa elimu kwa wananchi atumie bidhaa amabayo ipo ndani ya muda inaweza kupewa dawa ukatumia miezi mitatu iangalie kabla hujatumia ikiwa imeisha muda usitumie .

Habari Zifananazo

Back to top button