TMDA yagawa dawa za binadamu Magereza

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)Kanda ya Kusini imekabidhi msaada wa dawa tiba za binadamu zenye thamani ya shilingi milioni 15.9 kwa gereza la Wilaya ya Lindi mkoani Lindi.

Meneja wa Kanda wa TMDA Engelbert Mbekenga amesema dawa hizo zilikamatwa katika maduka ambayo hayana kibali cha kuyauza katika kaguzi zilizofanywa na Mamlaka hiyo hivi karibuni katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Mkuu wa Gereza Fadhili Donille ameshukuru Mamlaka hiyo kwa kuchagua kuwapa dawa hizo ambazo amesema  zitasaidia kuwapa matibabu wafungwa wagonjwa toka Gereza hilo ambalo ni la Wilaya.

Advertisement

Aidha ameeleza kuwa Gereza hilo ni la rufaa ya matibabu kwa wafungwa wagonjwa hivyo dawa hizo zitakuwa na msaada mkubwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *