DAR ES SALAAM; MAMLAKA ya Dawa na Vifaatiba (TMDA) imeondoa sokoni dawa duni ya macho aina ya “XSONE N” matoleo namba 69E00123 na 69D02323 inayotengenezwa na kiwanda cha Abacus Parenteral Drugs Limited(APDL) kilichpo Kampala, Uganda.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo, imesema kuwa matoleo ya dawa hiyo yamebainika kutokukidhi vigezo vya ubora hivyo ni matoleo duni.
Ilisema kutokana na kubainika kwa matoleo hayo mawili ya dawa duni, TMDA inawaelekeza wananchi waelekezwe kuangalia kwa makini lebo ili kutambua nambari za matoleo ya dawa tajwa na endapo wataona namba za matoleo hayo wasitumie dawa hizo ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea .