TNMC yatoa vifaa tiba kituo cha afya Makole

DODOMA: MSAJILI wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Agnes Mtawa, amewaongoza watumishi wa baraza kuadhimisha miaka 71 tangu kuazishwa kwa baraza hilo mwaka 1953 kwa kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 5 katika Kituo cha Afya Makole kilichopo jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo leo, Mtawa amebainisha baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na baraza hilo tangu mwaka 1953 kuwa ni pamoja na ukuaji wa baraza kutoka kuwa sehemu ya Wizara ya Afya na sasa ni taasisi.

Pia kuongezeka kwa idadi ya wauguzi na wakunga hadi kufikia 52,188 bila kusahau ujenzi wa mfumo wa kielektroniki wa kuhifadhi orodha na taarifa za wanataaluma, ujenzi wa kituo cha mafunzo katika mji wa Kibaha sanjari na mradi unaoendelea wa ujenzi wa ofisi kuu jijini Dodoma.

Habari Zifananazo

Back to top button