TNMC yawasimamisha tisa kutoa huduma

DODOMA – Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewasimamisha wauguzi na wakunga tisa na kutoa onyo kwa wengine nane baada ya kukiuka Sheria ya Uuguzi na Ukunga na Kanuni zake za mwaka 2010.

Mwenyekiti wa Baraza Prof. Lilian Mselle, amewaambia waandishi wa habari baada ya Baraza kuketi kwa siku mbili kusikiliza tuhuma zilizokuwa zikiwakabili wauguzi na wakunga kutoka mikoa mitano nchini.

Amesema, wauguzi na wakunga  wawili kutoka kituo cha Afya Mikanjuni Jijini Tanga wamesimamishwa kutoa huduma kwa kipindi cha miaka na mmoja mwaka mmoja kwa kosa la kushindwa kudumisha viwango vya taaluma na maadili. Pia wauguzi wanne  wa kituo cha Afya kibaoni Mjini Ifakara, wamepewa adhabu ya ONYO kwa kushindwa kudumisha viwango vya taaluma na maadili.

Wauguzi wafundwa kukabiliana na changamoto

Muuguzi wa hospitali ya Mji Geita, amesimamishwa kutoa huduma kwa kipindi cha mwaka mmoja, wawili miezi sita na mwingine amepewa onyo kwa kosa la kushindwa kudumisha viwango vya taaluma na maadili.

Katika Kituo cha Afya Nyakumbu Kahama, Wauguzi wawili wamesimamishwa miezi sita na wengine wawili wamepewa onyo kwa kushindwa kudumisha viwango vya taaluma na maadili.

Wauguzi wawili katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga wote wamepewa onyo kwa kushindwa kudumisha viwango vya taaluma na maadili. Adhabu zote zimetolewa chini ya Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya Mwaka 2010 kwa kuzingatia uzito wa kosa na ushiriki wa mtuhumiwa katika kosa husika.

Habari Zifananazo

Back to top button