VIJANA wanaofanya tafiti katika nyanja mbalimbali katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)wameagizwa kutoa matokeo ya tafiti zao ili kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Rai hiyo imetolewa leo na Dk,Irene Isaka ambaye ni Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kongamano linalohusu Maendeleo ya Teknolojia kupitia tafiti mbalimbali lililoandaliwa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kushirikiana na GIZ .
Amesema kuwa endapo watafiti vijana wakitoa matokeo ya tafiti zao kwa jamii serikali za nchi za EAC kila moja zinaweza kuchukua hatua za mabadiliko ya tabia nchi .
“Lazima sasa wasomi vijana wanapofanya tafiti zao wazitoe zisomwe ili serikali na jamii zichukue hatua katika kukabiliana na changamoto zilizoibuliwa”
Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ,Profesa Emmanuel Luoga amesema kuwa CENIT@EA ni kituo cha Umahiri kinachojihuisha na masuala ya Kompyuta na Tehama kinahusisha nchi zote za Afrika Mashariki kwa lengo la kuhakikisha masuala ya tafiti yanaibuliwa ili kutoa majibu sahihi ya changamoto za jamii na kuibua ajira.