Tomiyasu yupo sana Arsenal

ARSENAL wamethibitisha kuwa beki wao Takehiro Tomiyasu amesaini mkataba utakaomuweka klabuni hapo hadi June 2026.

“Ni ndoto kuchezea klabu hii”, amesema Tomiyasu mara baada ya kusaini kanadarasi hiyo.

Mjapani huyo alijiunga na Arsenal Agosti 2021 akitokea Bologna ya Serie A na tangu asajiliwe amecheza nafasi zote katika safu ya ulinzi, na kuifanya Arsenal kucheza mechi 73 katika michuano yote.

Advertisement

Tomiyasu, 25, alianza kucheza soka katika klabu ya Avispa Fukuoka Japan, ambapo aliendelea na soka la vijana kabla ya kucheza mechi 45 katika kikosi cha kwanza.

Tomi ameichezea nchi yake mechi 41, ambazo ni pamoja na kucheza kwenye Michezo ya Olimpiki ya nyumbani katika msimu wa joto wa 2021.

/* */