Toure kocha msaidizi Saudi Arabia

KIUNGO wa zamani wa Ivory Coast, Yaya Toure ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Saudi Arabia.

Toure 40 atafanya kazi na Roberto Mancini, ambaye alimsimamia Manchester City.

Mancini aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa Saudi Arabia mwezi Agosti na ameshaiongoza timu hiyo mechi nne tangu.

Toure, aliwahi kucheza City kwa miaka minane baada ya kusajiliwa mwaka 2010, alianza ukocha mwaka 2019 na Standard Liege ya Ubelgiji.

Kiungo huyo wa zamani wa Barcelona pia ametumia muda kufanya kazi na klabu ya Donetsk Olympic ya Ukraine, Grozny ya Urusi, na kama mkufunzi wa ‘academy’ ya Tottenham Hotspur.

Habari Zifananazo

Back to top button