Tozo miamala ya simu kufutwa

SERIKALI imekusudia kufuta tozo kwa siku kwa kila laini ya simuk kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji ili kuchochea matumizi ya kielektroniki katika miamala mbalimbali.

Bajeti ya serikali iliyowasilishwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba imependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa sura 437 na Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, sura ya 306

Mwigulu amesema, kufutwa kwa tozo hizo kutasaidia kufikia malengo ya ujumuishwaji wa wananchi
wengi kwenye mfumo rasmi wa fedha na pia kwa nchi kuelekea kwenye uchumi wakidijitali.

Advertisement

Amesema, Benki Kuu ya Tanzania
imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuongeza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kufanya miamala.

“Hatua hizo ni pamoja na
usasishaji wa Mifumo ya Malipo ya Taifa
(upgrading), ikiwemo kukamilika na kuanza kutumika kwa Mfumo wa Malipo wa papo kwa papo (TanzaniaInstant Payment System –TIPS),
na usimamizi thabiti wa mifumo ya malipo nchini.”Amesema.

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *