TP, Espérance hakuna kiingilio

KUELEKEA mchezo wa kesho TP Mazembe wakicheza mchezo wake wa kwanza wa African Football League (AFL) katika dimba la Benjamin Mkapa dhidi ya Esperance De Tunis, mchezo huo hautakuwa na kiingilio.

TP Mazembe wamechagua kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa na inakuwa faida kwa Tanzania kushuhudia michezo mingine zaidi ya Africain Football League ambayo inasimamiwa na FIFA pamoja na CAF.

Mchezo kati ya Tp Mazembe dhidi ya Esperance hautakuwa na kiingilio na hivyo kila mtanzania na mpenda soka anaweza kwenda kesho Benjamin Mkapa kuwaunga mkono TP Mazembe.

Habari Zifananazo

Back to top button