“Mkataba huu unatoa haki ya upekee ya kufanya majadiliano kwa Awamu ya Miradi iliyoanishwa kwenye Mkataba huo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12).
Msingi wa kutoa haki hii ya kipekee ni kuwezesha pande mbili kufanya majadiliano na kumpa uhakika Mwekezaji kujadiliana katika maeneo pasipo kuwepo kwa majadiliano na Mwekezaji mwingine katika maeneo hayo hayo.
Hivyo, iwapo kipindi hicho kitakwisha bila kufikia makubaliano, TPA inaweza kuanzisha majadiliano na Wawekezaji wengine katika maeneo hayo pasipo kuwepo kwa mgogoro wowote chini ya Mkataba huo…,” amesema Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Bungeni Jijini Dodoma akiwasilisha Azimio la kuomba bunge kuridhia Mkataba kati ya Tanzania na Dubai.