TPA kuimarisha ufanisi bandari zote

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Plasduce Mbossa amesema mamlaka hiyo inaendelea kufanya juhudi  kuimarisha ufanisi wa bandari zote nchini, ili kuchochea uchumi wa nchi na maeneo husika.

Mbossa alisema hayo jana, wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas ofisini kwake mkoani hapa.

Mbossa amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa dhamira ya TPA ni kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Mtwara kufungua fursa za kiuchumi mkoani humu kupitia Bandari ya Mtwara.

Kwa upande wake, Kanali Abbas ameipongeza TPA kwa juhudi kubwa ambayo mamlaka hiyo inafanya kuhakikisha Bandari ya Mtwara inakuwa na ufanisi mkubwa kuufungua mkoa wa Mtwara kiuchumi kupitia Bandari ya Mtwara.

Habari Zifananazo

Back to top button