TPA yaonya matumizi bandari bubu

WAFANYABIASHARA wameshauriwa kuacha kutumia bandari bubu badala yake watumie bandari zilizorasmi Ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Bandari ya Tanga, Masoud Mrisha wakati akitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 31.9 kwa Hospitali ya Wilaya ya Pangani.

Advertisement

Amesema kuwa kwa kuendelea kutumia bandari bubu kunasababisha kuikosesha mapato serikali na hivyo kushindwa kufikiwa Kwa malengo ya serikali ya kuleta maendeleo Kwa wananchi wake.

“Msaada huu unatokana na makusanyo ya mapato tuliyoyapata katika mwaka 2021/22 hivyo tumeona sehemu yake tuweze kurudisha kwa jamii Ili iweze kusaidia wananchi”amesema Mrisha.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Hassan Msafiri amesema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka ambao serikali inaendelea kufanya maboresho ya ukarabati wa majengo katika hospitali hiyo.

“Tunawashuku TPA Kwa msaada huu Sasa utaongeza hari ya watumishi kuweza kutoa huduma bora za matibabu Kwa wagonjwa wetu”amesema Dk Msafiri.

/* */