TPA yasaidia shule, hospitali Bukoba

MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA), imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi Shule ya Msingi Bunena Manispaa ya Bukoba vyenye thamani ya Sh milioni 14.8.

Pia TPA imetoa mashuka ya wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manispaa ya  Bukoba yenye thamani ya Sh milioni 3.9.

Akikabidhi misaada hiyo kwa viongozi wa manispaa ya Bukoba, Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Bandari kwa niaba ya Mkurugenzi wa TPA, Nikodemas  Mushi amesema msaada huo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachokipata.

Advertisement

Amesema kuwa TPA wana utamaduni wa kutoa shukurani kwa jamii katika nyanja za afya, elimu na huduma kwa jamii kama sehemu ya shukurani kwa jamii inayozunguka bandari na kusema kuwa Mkoa wa Kagera utaendelea kunufaika na  huduma bora za bandari.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Hamid Njovu amesema msada wa bando za mabati 10, mifuko ya saruji 200, matofali 2,000 pamoja na shuka 200 uliotolewa na TPA utapunguza changamoto zilizopo.

Akizungumzia hali ya miundombinu ya elimu katika Manispaa ya Bukoba, amesema sasa Manispaa ya Bukoba ina mahitaji ya vyumba vya madarasa 519, madawati 1038, pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo 30157.

“Tunaweza kusema tunashukuru sana jambo la kusisitiza ni kuwa wananchi waendelee kutunza miundombinu ya ya bandari, ili misaada kama hii iendelee kuja mfano katika hospital yetu ya Wilaya tunaendelea na ujenzi ambao utagharimu zaidi ya Sh bilioni saba.

“Kwa sasa huduma zinapatikana vizuri na ujenzi  unaendelea na uhitaji wa mashuka kwa sasa ni 350, hivyo tunashukuru sana kwa msaada huu, “amesema Njovu.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Mhule ya Msingi Bunena, Eva Kipfumu amesema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1973 kwa sasa ina wanafunzi 1,241, huku uhitaji wa vyumba vya madarasa  mapya ni 15.

“Msaada huu utatusaidia kujenga madarasa mawili, hivyo tutakabiliana na upungufu uliopo, lakini ili ujenzi huu uanze bado tunapungukiwa mawe,mchanga ,kokoto, mbao, misumari na rangi hivyo tunakaribisha wadau waweze kutuunga mkono, ili tupunguze changamoto ya uhaba wa madarasa kwa sasa tunavyumba 14 vya madarasa na tuna upungufu wa vyumba 15, “amesema Kipfumu.

 

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *